Wabunge wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo wametoka Bungeni kufuatia kauli ya mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga (CCM) kudai kuwa wabunge wa viti maalum wa chama hicho hawawezi kupata nafasi hiyo bila kufanya mapenzi na viongozi wa chama.

Mbunge huyo wa CCM alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia katika mjadala wa Wizara ya Katiba na Sheria, mjadala ambao ulijaa mvutano mkali kati ya wabunge wa upinzani na wa chama tawala.

Wabunge hao wamechukua uamuzi huo leo asubuhi baada ya Mbunge wa viti maalum Chadema, Sophia Mwakagenda kusimama kuomba muongozo akiungwa mkono na wabunge wanawake wa chama hicho akimtaka Mbunge huyo kufuta kauli yake.

Hata hivyo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson aliwataka wabunge hao wakae na kuendelea na mijadala ya Bunge, ndipo walipoamua kutoka nje ya Bunge kuonesha hasira yao.

Mwenyekiti wa Bazara la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe alizungumza na waandishi wa habari nje ya Bunge na kuahidi kutoa tamko kali.

Msikilize hapa Halima Mdee:

Dissertation crafting providers quality customised writers for get
Mussa Mapunda: 3 Za Azam FC Sawa, Bado Za Coastal Union