Serikali nchini, imewataka wamiliki wa Shule za msingi kusititisha kutoa huduma za bweni kwa wanafunzi kuanzia shule za ya awali hadi darasa la nne ifikapo mwishoni mwa muhula wa kwanza wa masomo mwaka 2023.

Hatua hiyo, inatokana na Waraka Namba 2 wa mwaka 2023 uliotolewa Februari 28, 2023 na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa, ukieleza kuwa shule yoyote itakayotaka kutoa huduma za bweni kwa wanafunzi wa awali mpaka dasara la nne watatakiwa kuandika barua maalum ya maombi.

Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa.

“Hairuhusiwi kutoa huduma ya bweni kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika, na kwamba waraka huo unaanza kutumika Machi mosi mwaka huu.” amesema Dk Mtahabwa.

Bweni

Maagizo hayo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na Wizara Novemba mwaka 2020 na hivyo kuzitaka shule zote zinazotoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Aidha, Serikali pia imepiga marufuku shule zote za msingi kuwa na makambi ya kitaaluma na badala yake kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji kwa kuzingatia kalenda za mihula, ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 7, 2023
Yacouba Sogne awajibu kwa vitendo Ligi Kuu