Wasimamizi wa Taaluma ya Maabara wa Mikoa, wametakiwa kusimamia utoaji wa huduma bora na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa.

Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dkt. James Kiologwe ameyasema hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe wakati wa mafunzo elekezi ya wasimamizi wa taaluma ya maabara wa mikoa yanayofanyika jijini Dodoma.

Amesema, ubora wa huduma unatakiwa kuambatana na wataalamu wenye maadili ya kitaaluma wenye kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa pamoja kama timu.

“Mnatakiwa kutambua kuwa mmechaguliwa kati ya wengi na pia mmeaminiwa, kipaumbele cha Serikali ni ubora wa huduma hivyo tunatarajia kila jambo litaenda kwa umakini ili kufikia malengo,”amesema Dkt. Kiologwe.

Amesema, “Nendeni mkajipime kama mnaona hamtoshi kweye hiyo nafasi mliyochaguliwa basi rudini kwa wasajili muwaeleze kuwa mimi hapa siwezi, kazi hii ni kubwa kwangu, ili akae mtu anayefaa lakini naamini hapa wote mliochaguliwa mnafiti”

Aidha, amewataka wataalamu hao kuhakikisha kuwa watu wasiosajiliwa wanafanya usajilib ili kuendelea kuboresha huduma za Afya pamoja na kudhibiti mapato ya Serikali.

Kwa upande wake, Msajili wa Wataalamu wa Maabara nchini, Mary Mtui amesema mafunzo hayo yatawapa uwezo wa kujua namna ya usimamizi shirikishi, kwakusaidia kuimarisha na kusimamia eneo hilo pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria.

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku mbili, yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka wizara ya Afya, Mkurugenzi idara ya Afya OR – TAMISEMI na watumishi kutoka wizara ya Afya akiwemo msajili baraza la wataalamu wa maabara.

Msomera 'wachekelea' mawasiliano
Wachoma majengo ya Bunge wakilalamikia hali ngumu