Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Singida Big Stars Hussein Masanza amesema, kikosi chao hakina budi kuangalia mbele na kusahau kilichotokea Ijumaa (Februari 03) jijini Dar es salaam.

Singida Big Stars ilipoteza dhidi ya Simba SC kwa kufungwa 3-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa, hali ambayo ilikuwa tofauti na matarajio yao kabla ya Mtanange huo, ambao ulisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka la Bongo.

Masanza amesema Wachezaji na Benchila Ufundi wameanza kujipanga kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa mkoani Mbeya Jumapili (Februari 12), huku malengo yao makuu ni kupata alama tatu muhimu.

Amesema kilichotokea walipocheza dhidi ya Simba SC ni kukosa bahati sambamba na kuzidiwa mbinu na wenyeji wao ambao walionekana kuwa bora zaidi kwa nyakati fulani ndani ya dakika 90.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi dhidi ya Simba SC lakini bahati haikuwa kwetu, tumepoteza, hivyo ni jukumu letu kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao.”

“Ushindani ni mkubwa lakini bado ligi inaendelea, kazi yetu ni kuhakikisha tunatoa burudani na kupata ushindi kwa ajili ya timu na mashabiki wetu, ambao siku zote wamekua nasi kwa shida na raha.” amesema Hussein Masanza

Singida Big Stars inaendelea kukaa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikifikisha alama 43, sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na uwiyano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Young Africans yachimba mkwara mzito CAF
Chris Brown achefukwa, awatolea povu zito waandaji tuzo za Grammy