Aliyekuwa Mbunge ya Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye kwasasa ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lazaro Nyalandu amesema kuwa hatarajii kurudi jimboni kwake na hajawahi sema kuwa ana nia ya kugombea nafasi yoyote.

Amesema kuwa alikwenda kijijini Itaja, Wilayani Singida kuongea na viongizi wa vijiji na vitongoji kuhusu zoezi linaloendelea nchi nzima la CHADEMA kuwatambua na kuwaandikisha wanachama wao.

Nyalandu amesema kuwa muda mfupi baada ya kuanza kikao walivamiwa na watu ambao hawakuwatambua kwa wakati ule na walikuwa na silaha ambao waliondoka nao hadi ofisi ya Takukuru Mkoa wa Singida.

“Kama ilivyoripotiwa, kikao chetu cha ndani, kilivamiwa na watu ambao hatukuwafahamu, wakiwa na silaha na kuamrisha mimi, pamoja wenzangu wawili (David Jumbe na Mwenyekiti wa CHADEMa Kata ya Itaja, ndugu Peter) tuondoke nao,” amesema Nyalandu.

Aidha, amesema kuwa walimchukua kila moja wao katika chumba tofauti na kuwahoji juu ya uhalali wa kikao hicho cha CHADEMA, na kudai kuwa kulikuwa na harufu ya rushwa na baada ya mahojiano, waliwapeleka katika kituo kikuu cha Polisi Singida, na muda mfupi baadae wakasikia taarifa ya Takukuru Singida kuwa wao wamejiridhisha hapakuwa na tatizo na wamewakabidhi mamlaka ya Polisi.

Mei 27, 2019 waziri huyo wa zamani wa maliasili na utalii na wenzake David Jumbe na Mwenyekiti wa Chadema kata ya Itaja, Peter Mwangu walikamatwa na Takukuru wakituhumiwa kutoa rushwa na kufanya mkutano wa ndani bila kibali.

Makala: Chissano amwaga almasi kwa kiburi, JK ameishtukia, JPM amefunga…‘Kiswahili dili’
Wapinzani wamkalia kooni Netanyahu

Comments

comments