Rapa Stamina ambaye amefanya singo ya Kibamia na Roma Mkatoliki ameshangazwa na hatua kali zilizochukuliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kumuweka kitanzini Roma kujihusisha na sanaa hiyo kwa muda wa miezi sita.

Stamina ameshangazwa sana na maamuzi hayo kwani hapo awali Waziri huyo aliwaita na kuwapa onyo ya kufanyia marekebisho wimbo huo ndani ya miezi sita.

Amesema tangu kutoka kwa wimbo huo na tangu wapewe onyo la kufanya marekebisho ya wimbo huo mpaka sasa ni miezi mitatu yaani wapo ndani ya muda waliopewa kufanya marekebisho hayo.

“Kibamia ilitoka Novemba 22, 2017 na BASATA Roma Mkatoliki tuliitwa Disemba 6, 2017 na Mhe. Waziri akasema wametupa miezi sita na leo ndio kwanza Machi 1, 2018 mbona miezi sita bado au miezi sita ya Tanzania iko tofauti na kalenda ya dunia nzima? Mna tatizo gani na wasanii wetu BASATA na Wizara? Mnakuza au mnauwa sanaa? alihoji Stamina .

Stamina na Roma Mkatoliki kwa pamoja wanaunda kundi la ROSTAM ambao ndio wamiliki wa wimbo huo wa Kibamia lakini matokeo yake Roma Mkatoliki amechukuliwa adhabu peke yake kwa wimbo wa kundi hilo.

Madaktari bingwa waleta mgomo
Wastara atoa ripoti ya matibabu India, agundulika na tatizo jingine