Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi anatarajia kuachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la ‘Freedom’ siku chache zijazo.

Sugu ambaye anaendelea kudumu kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa muhula wa pili amesema kuwa ingawa yuko katika siasa, ataendelea kuachia nyimbo kwa lengo la kuutengeneza ‘brand’ zaidi na sio kujivunia mistari kama ilivyokuwa awali.

“Mimi bado mwanamuziki hata juzi nilikuwa studio narekodi ngoma mpya ambayo itasikika hivi karibuni, zamani tulikuwa tunajivunia mistarii lakini sasa hivi ni mambo ya Branding tu na kutoa video kali basi,” Sugu aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm.

Rapa huyo mkongwe alimsifia Fid Q kwa mabadiliko yake na uamuzi wake wa kufanya video kubwa akieleza kuwa sasa ameamua kuendana na namna ambavyo muziki wa sasa unavyotaka.

Mbinu Tano Zitakazoipa Ushindi Arsenal Mbele Ya Barca
Aggrey: Nimerejea Kuisadia Azam FC