Tailor Swift ameonesha kujibu matusi ya Kanye West kwa njia tofauti kupitia hotuba yake fupi aliyoitoa jana usiku baada ya kutajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Albam Bora ya Mwaka kwenye tuzo zenye heshima kubwa duniani, Grammy 2016.

Swift alivunja rekodi kwa kuwa mwimbaji wa kike wa kwanza kubeba tuzo hiyo mara mbili katika historia yake.

Kanye alimtusi Tailor Swift kwenye wimbo wake wa ‘Famous’ uliopo kwenye album yake ya ‘The Life of Pablo’.

“I feel like me and Taylor might still have sex / Why? I made that bi*ch famous.” Alirap Kanye kwenye wimbo huo.

Mwaka 2009, Kanye West alimpokonya tuzo Tailor Swift kwenye jukwaa la MTV/VMAs Awards akidai hakustahili tuzo hiyo.

Tailor Swift akipokea tuzo ya Albam Bora ya Mwaka

Tailor Swift akipokea tuzo ya Albam Bora ya Mwaka

Tailor amemjibu Kanye kwenye hotuba yake jana akiwaasa wanawake:

“Kama mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya Albam Bora ya Mwaka kwenye Grammy mara mbili, nataka kuwaambia wanawake wote huko nje, kutakuwa na watu njiani watakaojaribu kukata mafanikio yenu na msiwaache watu hao wawakatishe. Siku moja, utakapofika huko utaenda, utaangalia kila mahari na utatambua kuwa ulikuwa wewe na watu wanaokupenda waliofanya uwe pale. Na kwa hilo utakuwa na hisia kuu duniani. Asanteni kwa muda huu.”

Fahamu Kiasi cha Mshahara na Posho anazolipwa Rais Barack Obama
Mbunge avunja rekodi ya kubusu hadharani, apewa tuzo