Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji, unaofanyika Umoja wa Mataifa, New York, Machi 22-24, 2023.

Waziri Aweso amehutubia Mkutano huo Machi 22, 2023 ambapo amebainisha umuhimu wa dunia kukaa pamoja na kusimamia agenda ya maji; thamani ya maji katika maisha na uchumi; kuongeza uwekezaji katika eneo la maji; ushirikiano wa kimataifa katika maji; pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Katika mkutano huo, Tanzania imebeba agenda mbili ambazo ni utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Tatu (Water Sector Development Programe III), ambayo inahitaji Dola za Marekani Bilioni 6.47 katika kipindi cha 2022-2025.

Tanzania imejipambanua kwa agenda ya uwekezaji katika Sekta ya Maji ili kufikia Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Tanzania Water Investment Programme 2023-2030). Programme ambayo bado inaandaliwa na ipo hatua za mwisho kuzinduliwa inakadiriwa kuwa na bajeti ya zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 25 na itazinduliwa Mei 2023.

Makamu wa Rais ahimiza uzingatiaji maadili malezi ya Watoto
Tishio baa la njaa: CPB yawatoa hofu Wananchi