Aliyekuwa kiongozi na mwanamapinduzi ya kikomunisti wa Cuba, Fidel Castro amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 90.

Taarifa za kifo cha Castro zimetangazwa na Rais wa nchi hiyo, Raul Castro ambaye ni mdogo wake.

“Amiri Jeshi Mkuu wa mapinduzi ya Cuba amefariki majira ya saa nne na dakika 29 jioni hii (kwa saa za Cuba),” alisema Raul.

Fidel Castro ambaye alikuwa rafiki wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, aliongoza mapinduzi ya Cuba mwaka 1959 ambayo yalimuondoa madarakani dikteta Fulgencio Batista aliyekuwa akiungwa mkono na mataifa ya Maghariki hasa Marekani.

Mwaka 2006, alifikia uamuzi wa kumuachia madaraka mdogo wake Raul baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa kipindi kirefu.

Fidel Castro ni kati ya watu wachache duniani waliopata heshima ya kuwa na cheo cha juu zaidi cha kijeshi cha Field Marshall.

Apumzike kwa amani! Amina.

Gavana BoT: Hakuna Ubaya kuweka fedha kwenye ‘Fixed Deposit Account’
Aliyemwambia ‘mteja’ ataisoma namba kwa kumchagua Magufuli abanwa