Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesema kuwa Mabingwa wa Ligi hiyo, Young Africans SC na timu nyingine zilizoshiriki katika msimu ulioisha wa 2015/2016 zitakabidhiwa zawadi zao mapema mwezi ujao.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, ucheleweshaji wa kutoa zawadi hizo baada ya ligi kumalizika umetokana na baadhi ya timu zinazoshiriki kwenye mechi za mashindano ya kimataifa.

Allisema baadhi ya timu zimekuwa zikiendelea nae mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kuingia kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

“Tunaomba radhi kwa  timu husika, wachezaji na wadau wa soka kwa zoezi hili kuchelewa ila tunawahakikishia kuwa  zawadi ziko tayari na zitakabidhiwa  mwezi ujao,” alisema Nkurlu.

Nkurlu alisema kuwa Kampuni hiyo ya Simu itaendelea kutoa udhamini wa Ligi hiyo katika msimu ujao kama ilivyoainishwa katika mkataba kati yake na Shirikisho la Soka Nchini (TFF).

Video: Aeshi Hilaly hakubaliani na serikali kuwakata wabunge posho zao
Manji aendelea kumwagiwa Sifa, Pongezi kuishika Yanga