Tetemeko la ardhi, lenye ukubwa wa kipimo cha richa 6.1 limeipiga sehemu ya kaskazini mwa Uturuki, na kujeruhi watu wasiopungua 50.

Kiini cha tetemeko hilo kimerikodiwa umbali wa kilomita 170 mashariki mwa mji mkuu wa kibiashara wa Istanbul, ambako maafisa wamesema lilikuwa dogo kuliko 6.1 kwenye kipimo cha richa kama ilivyotangazwa na shirika la Marekani la kuchunguza matukio ya kijiolojia.

Baadhi ya wanafamilia wakiwa nje ya jengo wanaloishi wakijadiliana juu ya tetemelo lililoikumba nchi yao. Picha ya Ghettotext.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu aliyelitembelea eneo lililoathirika, amesema mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kuruka kutoka kwenye roshani ya jengo la ghorofa kutokana na kiwewe.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 24, 2022 
Mlipuko kituo cha basi wauwa wawili, wajeruhi