Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya viwanja kwa wachezaji wa timu ya Wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), na kupokea kombe la ubingwa wa COSAFA kutoka timu hiyo Ikulu Dar es Salaam.

Rais Samia ametoa zawadi hiyo leo, Oktoba 27, 2021 kwenye hafla ya kukabidhiwa kombe hilo na vijana hao ambayo imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo Rais Samia ametoa wito kwa Wanawake nchini kujitokeza na kushiriki katika michezo na kutumia fursa mbalimbali ikiwemo kujiendeleza katika mafunzo ya ukocha.

Aidha amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa wanamichezo wote nchini ili kuendelea kufungua fursa za ajira katika sekta ya michezo na burudani.

Rais Samia Suluhu pia amewataka Wachezaji kuendelea kufanya vizuri na kuitangaza Tanzania na vivutio vya utalii vilivyopo nchini, na wasanii kuendelea kudumisha mila na desturi zilizopo.

Mbaroni akifanya mapenzi na Mbuzi
Waliovujisha mitihani kuchukuliwa hatua- Dkt Gwajima