Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linamshikilia Emmanuel Zakaria (38) Mkazi wa Lusahunga Wilayani Biharamulo Mkoani humo kwa kosa la kufanya mapenzi na mbuzi jike mali ya Jacobo Nyawenda (37).

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Awadhi Haji, amesema wakati akiendelea na kitendo hicho ,ndipo alipita mke wa jirani yake na mlalamikaji na kumkuta mtuhumiwa anafanya mapenzi na mbuzi akatoa taarifa kwa wananchi wengine na mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi hao.

Wananchi walimkuta akiwa uchi akimfanyia Mbuzi kitendo hicho, walimkamata na kumkabidhi polisi, tunaye na tunaendelea kumhoji, lakini pia atapimwa afya ya akili ili kubaini kama hana tatizo ya ugonjwa wa akili na baadae hatua za kisheria zitafuta” amesema Kamanda Awadhi

Kamanda Awadhi amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi alikiri kufanya tukio hilo na kudai kuwa alizidiwa na tamaa za mwili. Amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na kwamba mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kituo cha polisi Biharamulo.

Twiga Stars wachangia Uwepo wa Vituo vya Michezo
Twiga Stars wadaka donge Nono