Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, amesema kumekuwa na wimbi la uporaji wa pikipiki maeneo tofauti jijini huku Kinyerezi, Kigamboni na Chanika Mwisho zikitajwa kukithiri kwa uhalifu huo, katika kile kinachoelezwa kuwa ni jitihada za kupambana na uhalifu. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetoa wito kwa madereva bodaboda katika Jijini la Dar es salaam, kuacha kuendesha  shughuli hiyo ifikapo majira ya saa 6 usiku.

Kamishna Simon Sirro, amesema kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia mwanya katika muda huo kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha pikipiki.

“Haiwezekani baa zifungwe saa sita halafu hawa wakashinda na kulala vijiweni hadi alfajiri, wanafanya nini? Ndiyo maana wanaibiwa pikipiki na wengine kutekwa,” amesema Kamanda Sirro.

Aidha, Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18 hadi 23 Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.

Kuhusu suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247 kutokana na oparesheni inayoendelea.

Alisema baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa mahakamani kwani upelelezi bado haujakamilika na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Rais Dkt. Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda wautosa mkataba wa EPA
Steven Nyerere: Nimetumia sanaa yangu na ujuzi wangu kumridhisha mama Sepetu