Mwigizaji na mchekeshaji mahiri Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho jijini dar es Salaam ambapo amekiri kwamba sauti iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, kweli ni yake na akifanya mazungumzo na mama Sepetu, Miriam Sepetu

Steve Nyerere amekiri na kusema hakufanya kwa nia mbaya bali ilikuwa kumridhisha mama Wema  Sepetu ili atulie.

Steve ametumia nafasi hiyo kuomba msamaha kwa Rais John Magufuli kwa kuwataja mawaziri wake kwenye sauti hiyo, pia amewaomba radhi mawaziri wote waliotajwa kwenye sauti hiyo pamoja na Chama cha Mapinduzi kwa yote yaliyotokea na ameahidi kwamba kamwe hataihama CCM.

”mimi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi, sifa ya kwanza nimekula kiapo cha kuitetea nilichokifanya ni kuanza kusema mengine kutumia sasa sanaa yangu na ujuzi niliopewa na mwenyezi Mungu ili kumridhisha mama atoke katika ile memorandamu yakumtoa mtoto na yeye mwenyewe wanahama chama” amesema Steven Nyerere.

Pia Steven amekanusha baadhi ya mambo ambayo Wema Sepetu alizungumza alipoita waandishi wa habari kujitangaza kuhama chama cha CCM na kuhamia Chadema.

Steven Nyerere amesema kati ya watu waliolipwa fedha nyingi kipindi cha kampeni 2015 ni yeye na Wema Sepetu.

”Dada (Wema Sepetu) haidai CCM hata senti tano, tusichume dhambi tumtangulize Mungu mbele” amesema Steven Nyerere

Hayo yamekuja siku chache baada ya sauti kuzagaa mitandaoni, Steve Nyerere akizungumza na mama Wema, akieleza jinsi alivyowashawishi wabunge waijadili ishu ya Wema kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya, na kumtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba anamuonea Wema.

Aidha amesema hana ugomvi na mtu yeyote, zaidi anaunga mkono mchakato wa Paul Makonda kupiga vita dawa za kulevya.

 

Uhalifu umekithiri Dar, boda boda mwisho saa sita
Rais mstaafu, Kikwete akutana na Rais Outtara wa Ivory Cost, wazungumzia hali ya elimu Afrika