Bifu kati ya meneja wa Arsenal Arsene Wenger na Jose Mourinho wa Man Utd limeendelea kudhihiri, baada ya wawili hao kukutana katika mkutano maalum  ulioandaliwa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Tovuti ya Gazeti la Marca la nchini Hispania muda mchache imeripita kuwa, wawili hao wameonyesha uhasama wao pale Arsene Wenger alipokataa kata kata kukaa sambamba na Mourinho wakati Sir Alex Ferguson alipokua akihutubia.

Taarifa hizo zimeongeza kuwa, wakati Mourinho alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa UEFA huko mjini Nyon nchini Uswiz aliomba kukaa kwenye kiti ambacho kilikua kitupu pembezoni mwa Wenger, lakini matokeo yake babu huyo wa kifaransa alikataa kwa kusema “Hapata jambo hilo halitowezekana.”

This handout picture released by UEFA shows (LtoR, front row) Juventus' coach Massimiliano Allegri, Manchester United's coach Jose Mourinho, UEFA Coaching Ambassador Sir Alex Ferguson, UEFA interim General Secretary Theodore Theodoridis, Bayern Munich's Carlo Ancelotti, Paris Saint Germain's coach Unai Emery and Real Madrid's coach Zinedine Zidane. (LtoR second row) UEFA Chief Refereeing Officer Pierluigi Collina, Gent's head coach Hein Vanhaezebrouck, Newcastle United's coach Rafael Benitez, FC Zenit's coach Mircea Lucescu, Arsenal's coach Arsene Wenger, FC Barcelona's coach Luis Enrique, Wolfsburg's coach Dieter Hecking, Dynamo Kiev's coach Serguei Rebrov, UEFA director of competitions Giorgio Marchetti and UEFA chief technical officer Ioan Lupescu posing for a picture during a session of the Elite football Club Coaches Forum at the UEFA headquerters in Nyon, on August 31, 2016Picha ya pamoja na maneja waliohudhuria kwenye mkutano wa UEFA hii leo, mjini Nyon nchini Uswiz.

Kufuatia hali hiyo mameneja wengine walionyesha kushangazwa na kitendo hicho na kumtaka Mourinho atafute mahala pengine pa kukaa, kwani bado kulikua na viti vingine vitupu.

Mameneja hao wamekua na uhasama wa muda mrefu kwa kutupiana maneno kupitia vyombo vya habari, na miaka miwiwli iliyopita walikaribia kizichapa hadharani, pale vikosi vyao vilipokua katika harakati za kusaka point tatu muhimu kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Serikali haijashindwa kuongoza nchi - Waziri Mkuu
Eden Hazard Ampiga Kijembe Mourinho, Amfagilia Conte