Matukio ya ujangili yamepungua kwa asilimia 70 kutokana na mafanikio ya kampeni ya kutokomeza vitendo hivyo iliyofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameaambia waandishi wa habari kuwa ingawa vitendo hivyo vimepungua, bado zipo nyara za Serikali ambazo zilifichwa na majangili awali.

“Wana akiba za pembe za ndovu na nyara nyingine za Serikali… lakini hasa wamewalenga tembo, wana akiba ya nyara hizo pamoja na ngozi za wanyama pori ambazo wanahangaika nazo jinsi ya kuzitorosha nje ya nchi,” alisema Dkt. Kigwangalla alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Aidha, Waziri Kigwangalla lieleza kuwa Serikali imechukua hatua madhubuti kuhakikisha inalinda sekta ya utalii inayoingiza fedha nyingi za kigeni ambayo kwa asilimia 90 inategemea wanyama pori.

Alitoa pongezi kwa vikosi maalum vilivyofanya kazi ya kuwasaka na kupambana na majangili pamoja na watu wengine wanaosaidia vitendo hivyo haramu.

Nape ashauri kuwepo ubunifu katika ulipaji kodi
Mohamed Morsi azikwa nchini Misri

Comments

comments