Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania bado ina maambukizi ya UVIKO 19, kwa sababu watu waliochanjwa hawajafikia asilimia 50%.

Amesema hayo katika ufunguzi wa Jengo la CCBRT jijini Dar es Salaam ambapo alikua akihutubia kabla ya mgeni rasmi Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Ummy amesema Jana Julai 4, 2022 kulikuwa na wagonjwa 7 na sita kati yao wametoka Dar es Salaam, huku Julai Mosi, 2022 wagonjwa walikua 32.

Ameongeza kuwa suala la uvaaji wa Barakoa linabaki kuwa na umuhimu kwa sababu watu waliochanjwa hajafikia asilimia 50%.

“Nchi za wenzetu wameacha barakoa na kutangaza kwa sababu wamechanja zaidi ya 70% ya watu wao, napata kigugumizi ninapoulizwa kuhusu kuacha barakoa au tusiache, tungekuwa tumechanja angalau 50% ningesema tuache,” ameongeza.

Rais Samia:Ubakaji wa watoto chanzo cha Fistula
NECTA yatangaza matokeo kidato cha sita