Mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Mnero, wilayani Nachingwea mkoani Lindi aliyetajwa kwa jina la Agnes Jeremiah, ameuawa kikatili na watu wasiojulikana.

Kamanda Renatha Mzinga

Kamanda Renatha Mzinga

Taarifa zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo zimeeleza kuwa mwanafunzi huyo alibakwa na wanaume wasiofahamika ambao baadae walimnyonga na kuutupa mwili wake kichakani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amewaambia waandishi wa habari kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na tabia za kutoroka bwenini usiku na kwenda kwa mpenzi wake wa kiume.

“Ni kweli taarifa ya kifo cha huyo mwanafunzi Agnes Jeremiah ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mandawa, akiwa bwenini huko Mnero Sekondari alitoroka usiku kwenda kwa mwanaume,” alisema Mzinga.

Kamanda Mzinga alisema kuwa Jeshi hilo linamshikilia Abdallah Ismail, mkazi wa kijiji cha Mnero Ngongo ambaye ni dereva wa pikipiki za abiria (bodaboda) kwa ajili ya mahojiano kuhusu tukio hilo.

Lulu, Richie waibeba Bongo Movies Kimataifa, Wanyanyua Tuzo AMVCA
Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu, Takukuru Waitiwa Ushahidi