Usain Bolt anaamini kuwa klabu yake pendwa ya Manchester United ndio itakayoibuka na Ubigwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Man United inayonolewa na kocha Jose Mourinho ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mpaka sasa.

Bolt ambaye ni mshindi  mara nane wa medali za dhahabu aliyestaafu riadha mwaka huu alionekana akiwa jukwaani akishuhudia mchezo baina ya Man Utd na Leicester City ambapo Man Utd waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Bolt anaamini United ndio watakao shinda ubigwa wa ligi kuu msimu huu tangu walipofanya hivyo mwaka 2013.

”Binafsi nafikiri tuko vizuri zaidi na wachezaji wanajiamini kitu ambacho ni muhimu zaidi siku zote” alisema Usain Bolt.

Usain Bolt ni shabiki mkubwa wa Man United

Jose Mourinho aliiwezesha Man United kushinda kombe la EFL na kombe la Europa League msimu uliopita lakini Bolt anakiona kikosi cha Man United kikobora zaidi huku akipendekeza kuongezwe wachezaji wengine wapya wawili.

Mwanariadha huyo amesema kurejea kwa Zlatan Ibrahimovic katika kikosi cha mashetani wekundu kutaongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji na kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri pia katika michuano ya klabu bingwa.

 

 

 

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 6, 2017
Video: Mgombea wa urais alala mahabusu siku nne Dar, Ukawa wasusa, CCM wala