Operesheni tumbua majipu imehamia ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambapo baadhi ya viongozi wake wamefukuzwa, kusimamishwa na wengine kushtakiwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ngazi ya Taifa, Abdulrahman Kinana.

Akieleza kuhusu maamuzi ya Baraza Kuu ya Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma mbalimbali, ilibainika kufanyika kwa ufisadi na udanganyifu katika miradi ya chama hicho iliyo chini ya Jumuiya hiyo.

Alisema kuwa uchunguzi huo ulibaini kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda ambaye sasa ni Mbunge wa Mbinga Mjini, alihusika kuwashawishi viongozi wa ngazi ya chini kufanya ufisadi na udanganyifu katika kuuza shamba la ekari 210 la UVCCM lililopo Igumbilo, Iringa vijijini.

“Mapunda hakutoa taarifa ingawa kulikuwa na vikao vingi vya kamati ya utekelezaji na Sekretarieti kuhusu shamba la Igumbilo, alipokea fedha za mauzo kwa aliyekuwa Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Ali Nyawenga,” alisema Shaka.

Alisema kuwa Mapunda alichukua hati ya kiwanja hicho bila idhini ya vikao husika na akaiuza kwa kuibadilishia matumizi.

Alieleza kuwa baada ya uchunguzi, imebainika kuwa alifanya udanganyifu hivyo jina lake limefikishwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa ajili ya hatua stahiki. Mwingine aliyefikishwa kwa Katibu Mkuu wa CCM ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga na Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Elisha Mwampashi.

Shaka aliwataka waliofukuzwa kwa tuhuma mbalimbali kuwa ni pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Ally Nyawenga na Katibu Muhtasi wa ofisi ya UVCCM mkoa wa Iringa, Upendo Kinyunyu.

Wapinzani Zambia walia kuibiwa kura, Rais Lungu aongoza matokeo ya awali
Ni Usain Bolt Tena, Atwaa Medali Ya Tatu Mfululizo