Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetangaza kufanya mikutano ya hadhara tarehe 1 Septemba 2016 kwa nchi nzima. Akitoa tamko hilo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amewataka wanachama wote, viongozi wa chama, wabunge, na mabaraza yote ya chama, madiwani wote nchi nzima kuandaa mikutano ya ndani ya chama katika ngazi zote.