Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amekabidhi daipa elfu 85,000 kutoka Taasisi ya GSM Foundation katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.

Mjema amesema kuwa Daipa hizo zitagawiwa katika vituo vya afya 26 vya wilaya yake ambapo wazazi wenye watoto wanaohudhuria kliniki na wale watakaojifungua hivi karibuni watakabidhiwa.

Pia amewapongeza GSM Foundation huku akiwataka wadau wengine waige mfano huo, na kuwaomba GSM Foundation waendelee kuwasaidia kwani yapo masuala mbalimbali ya kiafya yanayohitaji msaada wao.

Man City Kumpigania Sergio Aguero
Roberto Martinez Azomewa Hadharani