Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ali Hapi amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, ambapo amemtaka kuendeleza miradi yote iliyopo ndani ya wilaya hiyo.

Hapi amekabidhi ofisi jijini Dar es salaam, alipokuwa akiwaaga viongozi na watumishi mbalimbali aliokuwa akifanya nao kazi.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi hao, amewashukuru kwa ushirikiano waliompatia wakati wote wa uongozi wake ndani ya wilaya hiyo.

“Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mlionipa kwa muda wote wa uongozi ndani ya wilaya ya Kinondoni,”amesema Hapi

Video: Makonda azigeuki mali za umma, waliotaifisha sasa kunyang'anywa
Jinsi ya kujiandaa vizuri kwa 'interview' ya kazi

Comments

comments