Chama cha Tanzania Labor Party (TLP) kimewataka wananchi wa Zanzibar kuilinda na kuitunza amani iliyopo kwa kutoyumbishwa na maneno ya wanasiasa ambayo yana nia ya kuchochea vurugu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama hiko Mh. Agustino Mrema amesema kwamba kauli za baadhi ya viongozi visiwani humo zina lengo la kupoteza amani iloyopo.

Aidha Mrema amesema kwamba amani ya Zanzibar ikiharibika hata bara haiwezi kuwa salama, hivyo ni vyema kauli za kuvuruga amani zisizingatiwe ili kulinda maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

VIDEO: MAGAZETI LEO 27 MAY 2016
MREMA: WAZANZIBAR ILINDENI AMANI YENU

Comments

comments