Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif ametoa tuhuma kali dhidi ya Prof. Ibrahimu Lipumba kuwa ana lengo la kukivuruga chama na anakihujumu kwa makusudi kwa kutumiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Maalim ametoa kauli hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa kwa sasa Prof. Lipumba hana mamlaka na chohote ndani ya Chama cha CUF kwakuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limemchukulia hatua za kinidhamu.

Amesema hana ugomvi na Prof. Lipumba na yuko tayari kukaa naye meza moja kueleza uongo wa mtaalamu huyo wa uchumi ikiwa ni pamoja na ukweli anaouficha kuhusu kujiuzulu kwake kwenye nafasi ya uenyekiti wa CUF.

Aidha, mbali na kukiri kuwa CUF inapitia katika wakati mgumu kwa sasa, Maalim amesema kuwa hujuma anazozifanya Lipumba, zinatokana na wakubwa kuchukizwa na kitendo cha chama hicho kuwasilisha vielelezo mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC) vinavyo watuhumu viongozi wa Serikali kutumia mamlaka yao vibaya katika uchaguzi mkuu mwaka jana.

Kama uliikosa haya mahojiano ya Dar24 na Naibu Katibu Mkuu wa CUF

Video: Atakaye maliza mgogoro CUF ni watu wawili tu.. – Sakaya

Makonda kusafisha uwanja wa fisi
Video: Chadema yataja siri tano mafanikio ya Ukuta, Janja ya Maalim Seif hadharani