Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amechangia kiasi cha shilingi milioni 5 katika ujenzi wa ofisi za CCM Kata ya Kiwangwa iliyopo jimboni humo.

Amesema kuwa ni wajibu wa kila mwanachama wa chama hicho kuchangia maendeleo na kuimaarisha chama ili kiweze kuwa imara zaidi.

“Viongozi wangu wa Kata ya Kiwangwa walinifuata na kunieleza wanataka kujenga ofisi ya CCM Kata, nikasema CCM ndio sisi na tunawajibu wa kukijenga chama chetu,”amesema Ridhiwani Kikwete

Sababu kwa nini nywele zako hazikui
Makala: Kwanini Nikki wa Pili anaweza kuwa Rais, kwanini hawezi