Wataalamu wa afya wamesema ingawa teknolojia ya kisasa imeboreshwa, lakini kadri muda unavyozidi kwenda watu wengi wanaishi maisha bila ya kufanya mazoezi ya kutosha, aidha ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na shirika la moyo la Marekani lilieleza kwamba mabadiliko ya kiuchumi, watu kuhamia mjini , ustawi wa viwanda na kuenea kwa biashara za kimataifa huleta mabadiliko ya maisha .
Hayo yamesemwa na mtaalamu wa afya kutoka chuo cha Sayansi Muhimbili Dk, Fredy L. Mashili alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Oktoba 4, 2016 jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo iliyotokewa imeonyesha kuwa watu wengi wanaokaa maofisini kwa muda mrefu wako hatarini kupata magonjwa mbalimbali. Bofya hapa kutazama video