Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewatoa hofu Watumishi na kuwaeleza kuwa mambo yanaenda vizuri kuhusu safari ya kuhamia Dodoma na kuwataka watambue kuwa safari tayari imeiva na kikubwa ni kwamba safari itakuwa kwa awamu kama ambavyo imepangwa.

Majaliwa ameongea hayo alipokutana na kuzungumza na watumishi wa Ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.  Bofya hapa kutazama video #USIPITWE

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi  zilizoko chini ya Ofisi yake baada ya kuzungumza na watumishi wa Ofisi yake kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, Agost 17, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana  Ajira na Walemavu, Jenista  Mhagama , Wapili kulia kwake ni Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira  na Vijana, Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu baada ya kuzungumza nao  kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam Agost 17, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana  Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, Wapili kulia kwake ni Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira  na Vijana, Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi.
Malinzi Amlilia Joao Havelange
Majaliwa: Safari ya Dodoma imeiva, Awataka Watumishi Ofisi yake Kujiandaa