Wapiganaji wanaodaiwa kutoka Uganda wameshambulia kambi ya Umoja wa Mataifa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuua mmoja wa wanajeshi wanaolinda amani.

“Ninaweza kuthibitisha kwamba kumetokea shambulio katika kambi ya Monusco eneo la Mamundioma asubuhi hii na mlinda amani mmoja amefariki na wengine 12 kujeruhiwa”, alisema Florence Marchal ambaye ni msemaji wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Msemaji mmoja wa jeshi amelituhumu kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika kijiji kimoja karibu na mji wa Beni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wanajeshi wa DR Congo walikabiliana na waasi hao wa AFD kutoka Uganda eneo hilo siku ya Jumapili.

Siku moja awali, wapiganaji wa ADF ambao wamekuwa wakiendesha harakati zao karibu na mpaka kati ya DR Congo na Uganda walishambulia wahudumu 10 wa uchukuzi wa abiria wanaotumia pikipiki.

Video: Shirika la posta laipiga jeki taasisi ya moyo (JKCI)
Rais wa Misri amshukuru Salah, atoa zawadi nono