Wabunge wanne wa nchini Kenya, wameshtakiwa kwa kukutana kinyume cha sheria na kushiriki maandamano dhidi ya Serikali ya Rais, William Ruto kuhusu kupanda kwa gharama za maisha.

Wakili wao Danstan Omari, alisema Wabunge waliokamatwa ni pamoja na viongozi wa kundi la Odinga katika mabaraza yote mawili ya bunge, lakini waliachiliwa kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Nairobi.

Sehemeu ya waandamanaji waliojitokeza Machi 20, 2023.

Awali akizungumza na vyombo vya habari hapo jana Machi 23, 2023, Odinga alitaka kuachiliwa huru kwa wabunge hao, na kuonya kuhusu vitisho vinavyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano ya Kenya, ya kufuta leseni za vituo sita vya televisheni vilivyo ripoti maadamano.

Aidha, amesema ataendelea kuitisha maandamano hayo mara mbili kwa wiki, kuitaka serikali kukabiliana na kupanda kwa gharama za vyakula vya msingi kama vile unga wa mahindi ambao umesababisha mfumuko wa bei na bidhaa kuwa juu.

Wabunge wa Azimio ambao mara baada ya kukamatwa walihamishwa kutoka Kituo cha Polisi cha KICC hadi Kituo cha Central na kisha Kituo cha Polisi cha Kiambu. Picha ya Kenya Report.

Odinga, pia anamshutumu Ruto kwa udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana (2022), ambao alishiriki kwa mara ya tano mfululizo kugombea nafasi ya urais nchini Kenya, na alipinga matokeo hayo Mahakamani.

Hata hivyo, mtu mmoja aliuawa na wengine zaidi ya 200 walikamatwa wakati walipokuwa wakishiriki maandamano hayo yaliyohamasishwa na Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga siku ya Jumatatu Machi 20, 2023.

Mbuge: Mikoa ianzishe timu ya Wataalam kukabili maafa
Serikali yataka Wananchi kutumia fursa, kufanya kazi kwa bidii