Wabunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametangaza kuhamia chama cha NCCR Mageuzi mara baada ya bunge kumaliza muda wake Juni 19 mwaka huu.

Wabunge hao ambao ni Joyce Sokombi na Susan Masele wametangaza uamizi huo leo Jijini Dodoma, wametaja sababu za kufikia uamuzi huo ni pamoja an madai ya katiba ya CHADEMA na kuvunjwa na baadhi ya wanachama kufukuzwa uanachama bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

”Kuna unyanyasaji dhidi ya wanawake na madaraka kuhodhiwa na wanaume hivyo kusababisha unyanyasaji wa kijnsia wa kingono” amesema Susan

Ameongeza kuwa ndani ya chama hicho kunamakundi ya kibaguzi huku wengine wakionekana wapiga makofi bungeni na wengine wakiwa wachangiaji Bungeni.

Mapema mwezi huu wabunge wawili wa CHADEMA walitangaza kukihama chama hicho mara baada ya bunge kumaliza muda wake wabunge hao ni Joseph Selasini mbunge wa Rombo na Anthony Komu mbunge wa Moshi vijijini.

Kovu lisilofutika: Miaka 24 kuzama kwa MV Bukoba

TARURA yarekebisha madaraja yaliyosombwa na mvua, Dodoma, Manyara

Video: Polisi -"Hatujifichi na tochi kukomoa madereva"
Ulinzi na Usalama sherehe za Eid el Fitri waimarishwa