Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amewasimamisha kazi vigogo wawili wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Makao Makuu na Bandari ya Kiwira Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na kuagiza wapangiwe majukumu mengine.

Waitara amechukua uamuzi huo kwa madai ya uwepo wa uzembe wa kutotoa taarifa za tatizo kuhusu ubovu wa meli ya Mv Mbeya II tangu iliporipotiwa mapema mwaka 2020 na kiongozi wa meli hiyo na mabaharia.

Waliosimamishwa kazi ni Kapteni wa meli kutoka makao makuu TPA, Abdalla Mwengamno na Kaimu Meneja wa Bandari Ziwa Nyasa, Hamis Nyembo.

“Mlikuwa mnatambua changamoto ya meli hii tangu mwaka jana lakini hamkutoa taarifa jambo ambalo limehatarisha usalama wa wasafiri wanaotumia meli hiyo,” amesema Naibu Waziri.

NEC yatangaza uchaguzi
Huu ndiyo utaratibu wa kusafirisha makinikia - Majaliwa