Mkuu wa Mkoa Katavi, Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga ametakiwa kupeleka wakaguzi wilayani Mlele na kubaini watu waliokula fedha za chama cha ushirika cha Ukonongo na kuwachukulia hatua.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana (Jumatatu, Agosti 22, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Inyonga wilayani Mlele.

“Watakaobainika watiwe hatiani. Licha ya bodi ya ushirika huo kuvunjwa, hatuwezi kuacha suala hili limalizike kwa kuvunja bodi kwa sababu walioingia wanaweza kuiba kwa mategemeo ya kuvunjwa bodi,“ – Majaliwa

Majaliwa amesema kila mtumishi afanye kazi na awajibike kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kwa mujibu wa taaluma yake ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwani hilo ndilo lengo la kuajiriwa kwake.

“Haiwezekani hapa kuna Ofisa Ushirika halafu Waziri Mkuu analetewa mabango ya kumtaka atatue tatizo la chama cha Ushirika. Hali hii inaonyesha hapa hakuna kazi inayofanyika,“ – Majaliwa

Pia amesema wanahitaji watumishi watakaosikiliza maelekezo yanayotolewa na Serikali na kuyafanyia kazi kwa sababu malengo ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ni kuona nchi hii inabadilika hivyo wasioweza ni vema wakaandika barua za kuacha kazi.

 

 

 

Mabomu ya Machozi yaiamsha Moshi
Kamanda Siro afunguka kuhusu 'kubomoa UKUTA'