Watangazaji wawili wa Televisheni waliotajwa kwa majina ya Krystin Lisaius (26) na Somchai Lisaius (42) wanakabiliwa na kifungo jela kwa kosa la kumdhuru mtoto wao wa miezi minne kwa dawa za kulevya aina ya ‘Cocaine’

Wawili hao wakazi wa Arizona, Marekani ambao ni wanandoa wanadaiwa kuwa walitoka kutumia dawa hizo za kulevya katika sherehe moja ya anasa zinazoambatana na matumizi ya dawa mbalimbali za kulevya, baadae ndani ya saa 12 mama alikinyonyesha kichanga hicho.

Kwa mujibu wa Tucson Weekly, baada ya kumnyonyesha waliona hali ya mtoto inakuwa mbaya ndipo walipoamua kumkimbiza hosptalini ili kumnusuru.

Hata hivyo, wazazi hao waliposhauriwa na daktari kumchukulia vipimo zaidi mtoto wao kuona kama amepewa kitu kisicho cha kawaida walionesha kugoma hadi mtoto alipoendelea kuzidiwa na kukosa fahamu, ndipo waliporuhusu apelekwe kwenye hospitali nyingine maalum kwa watoto.

Baada ya kumfanyia vipimo vya kina, mkojo wa mtoto huyo ulionesha kuwa na dawa za kulevya aina ya ‘Cocaine’.

Awali, wawili hao walikana kutumia dawa za kulevya lakini walikiri baadae kuwa hutumia dawa hizo kila baada ya wiki sita.

Polisi wa Arizona walipekua nyumba ya wazazi hao na kukuta mzigo wa dawa za kulevya aina ya cocaine wenye ujazo wa gramu 1.9.

Wamefunguliwa mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, kumdhuru mtoto pamoja na kukutwa na dawa za kulevya. Kwa shtaka la kumdhuru mtoto kwa dawa za kulevya wanaweza kutupwa jela kwa kipindi kisichopungua miaka miwili kila mmoja.

Nay Wa Mitego Atokwa Na Povu, Ni Baada Ya Shamsa Ford Kuolewa, Amchimba Mkwara Mwanaume Aliyemuoa
Mugabe; Nilikufa Halafu Nikafufuka