Benchi la Ufundi la Azam FC, limeanza kupunguza baadhi ya wachezaji wake msimu huu ili kuongeza nyota watakoimarisha kikosi hicho msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia Dar24 Media baadhi ya wachezaji wanaoweza kukutana na panga hilo ni Yahya Zayd, Ismail Kada na Cleophace Mkandala.

Kocha wa Azam FC, Kali Ongala, alikiri wamepanga kuwaacha baadhi ya wachezaji wao, ingawa hakuwataja majina.

Kocha huyo amesema atakaa na uongozi wa klabu hiyo kupanga mikakati ya kupata nyota wapya watakaokiongezea nguvu katika kikosi hicho msimu ujao.

“Wapo wachezaji ambao tutawaacha kuweza kuwapa nafasi ya kulinda vipaji vyao katika timu zingine, tutasajili kuhakikisha wachezaji wazuri zaidi tunapata kikosi bora,” amesema.

Kikosi hicho hivi sasa kimebakisha michezo miwili katika mashindano yote msimu huu.

Azam FC itachuana na Polisi Tanzania kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kabla ya Jumatatu ijayo kuvaana na Young Africans katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga katika fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Dkt. Tulia awashukia wapotoshaji ukodishaji Bandari
Waarabu kumtajirisha Karim Benzema