Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na watoto Dkt. dorothy Gwajima ametuma salamu kwa watendaji wa Mtaa wa Ghana Mkoani Mwanza ambao  yupo mtoto aliyenyimwa haki ya kwenda shule.

Ameyasema hayo alipokuwa ametembelea Wilayani Tarime Mkoani Mara katika kituo cha Nyumba salama cha Masange kinachotumika kuwalea watoto waliokumbwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia au walio katika hatari ya kukumbwa na vitendo hivyo.

Hii imejiri baada ya vyombo vya habari kuripoti juu ya mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Shamsa Ramadhani mwenye umri wa miaka tisa ambaye amebeba jukumu la kumuuguza bibi yake kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ilihali baba yake yuko hai na hajawahi kumuona.

“Pale Mwanza naenda huko kesho kutwa mtoto ameachishwa shule ana miaka 9 anamuuguza bibi yake eti system haijui wanafanya nini pale kama wewe ni kiongozi huna mbinu za kusikiliza taarifa ya habari, kusoma taarifa mbalimbali wewe ni tatizo, Mwanza mwambieni, Mtendaji wa Mtaa, Kata, ambayo yupo mtoto aliyenyimwa haki ya kwenda shule, ana miaka tisa pamoja na akili yote hiyo haendi shuleni watendaji wametulia tulia wanasubiri ndugu wajitokeze nakuja Mwanza,” Amesistiza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima ameitaka Jamii kushiriki kikamilifu kufuatilia matatizo yanayowakumba wanajamii husika na kama wanashindwa kufanya hivyo wanakuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine na vitendo hivyo

IGP Sirro atoa msimamo agizo la kumkamata Askofu Gwajima
Uganda kuwapokea wakimbizi 2000 wa Afganistan