Watu wawili wamefariki dunia papohapo na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyosababishwa na lori lililowafuata abiria katika kituo cha daladala Kimara Suka jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo amesema watu hao walikuwa wakisubiri usafiri katika kituo hicho.

Amesema ajali hiyo iliyosababishwa na lori imehusisha na baadhi ya vyombo vingine vya usafiri ikiwemo daladala, bajaji na pikipiki.

“Watu wawili wamefariki dunia na wanane wamepata majeraha wengine wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wengine wamepelekwa Mloganzila,” amesema Kamanda Murilo.

“Ukiangalia chamzo ni uzembe wa dereva ambapo aliona wenzake wamesimama kwenye kivuko yeye akapita na kusababisha ajali hiyo.” Alisema kamanda Murilo.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango ambaye aliyefika eneo la tukio na katika mahojiano yake na Mwananchi amesema ajali hiyo imehusisha watu na vyombo vya usafiri.

Mashuhuda wa ajali hiyo pia wakizungumza na Dar24 wamesema chanzo cha ajali ni lori ambalo lilikwenda kwa kasi katika eneo la kivuko cha waenda kwa miguu na kusababisha vyombo vyabusafiri vilivyokuwa mebel yake kugonga abiria waliokuwa kwenye kituo hicho cha daladala.

Lowasa taabani Muhimbili
Chris Brown ashitakiwa kwa kesi ya ubakaji