Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mara baada ya kuanza kurushuiana risasi na polisi hao.

Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma, Gemini Mushy amesema kuwa tukio hilo limetokea jana jumatano katika kijiji cha Nungungulu Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Aidha, Kamanda huyo amesema kuwa watu hao walikuwa na silaha aina ya SAR na risasi zake 41 pamoja na pikipiki ambayo namba zake zimehifadhiwa kwa sababu za kiusalama zaidia.

Amesema kuwa wakiwa katika doria waliona pikipiki ikiwa imepakiwa kitu ambacho kiliwafanya wasimame ili kuikagua, ndipo abiria alitoa bunduki na kuanza kuwashambulia askari ambao nao walianza kujibu mashambulizi na kufanikiwa kuwazidi maarifa hivyo kupoteza maisha.

Hata hivyo, Kamanda Mushy amewata wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utumiaji wa silaha kama wanawafahamu au wanapowatilia shaka.

Wanawake jinsi ya kuutambua ugonjwa wa 'Fibroids'
Jorge Celico abebeshwa zigo la kufuzu kombe la dunia