Waziri wa Nchi ofisi ya Rais – TAMISEMI, Seleman Jafo, kwa masikitiko ametangaza kifo cha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamisi Iddi Malinga kilichotokea jana Juni 14, mkoni Manyara.

Waziri Jafo ametoa pole kwa uongozi wa mkoa wa Manyara, wilaya ya Babati na halmashauri ya wilaya ya Babati, wananchi, familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huo.

Marehemu Malinga, aliteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kushika nafasi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati, Julai 12, 2016.

Kabla ya uteuzi huo aliwahi kufanya kazi sehemu mbalimbali nchini, na ndani ya CCM, Waziri Jafo amesema Serikali itaendelea kutambua mchango wake katika maendeleo ya nchi.

Baba mbaroni kwa kuozesha mtoto wa miaka 12, "waliokula hela za ushenga kuzitapika"
Serikali yapiga marufuku Mgonjwa kudaiwa damu kabla ya huduma