Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangallah amepata ajali ya gari akitokea jijini Arusha kabla ya kufika katika eneo la Magugu na hali yake ni mbaya.

Aidha, Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flaitey Masai amesema kuwa Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni Mwandishi wake wa Habari amefariki dunia.

“Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amepata ajali akitokea Arusha hali yake ni mbaya na tunasubiri Helicopter ili tumhamishe Hospitali na Mtu mmoja ambaye inadaiwa ni Mwandishi wake wa habari amefariki dunia,” amesema Mbunge wa Mbulu Vijijini Flaitey Masai

 

 

Video: Kauli ya JPM yamvuruga RC Makonda, Mkurugenzi Twaweza aibuliwa zengwe la uraia
Zoezi la uhakiki wa leseni lasitishwa