Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya Madawati ya shule za Dar es salaam kutoka Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ikishirikiana na Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora nchini.

Waziri amekabidhiwa madawati hayo katika shule ya msingi Chamazi jijini Dar es salaam mapema leo Julai 28, 2016.

IMGS8101Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo kukabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salaam  Julai 28, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke  Felix Lyaviva.

IMGS8109Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wananchi wa Temeke baada ya kuwasili kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi kukabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100  kwa ajili ya Shule za Dar es salam  Julai 28, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

IMGS8131Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait  nchini, Jaseen Al Najem  na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chamazi wakiwa wamekaa kwenye  madawati mawili kati ya 300 yaliyotolewa na Kuwait ili kukabiliana na tatizo la madawati jijini Dar es salaa. Makabishianoni hayo yalifanyika kwenye  Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. Waliosimama watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, , Augustine Mahiga, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Susan Kolimba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

IMGS8158Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba.

IMGS8238Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , Balozi Augustine Mahiga (kulia kwake) wakifurahi  wakati , Bwana Murtaza Adamjee alipoongoza wimbo katika hafala ya kukabidhi madawati kwa mkoa wa Dar es salaam iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.

 

IMGS8262Baadhi ya wanafunzi na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu kwenye shule ya Msingi yaChamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.

IMGS8295Waziri Mlkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi, Augustine Mahiga (katikati) na Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora Nchini katika hafla ya kakabidhi madawati na fedha  shilingi milioni 100 kwa shule za Dar es salaam  iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016.

IMGS8353

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chamazi  jijini Dar es salaam baada ya kupokea madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam Julai 28, 2016.
Madawati ayo yalitolewa na Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ikishirikiana na Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora nchini.
Kigwangala Akutana Na Viongozi Wa Mfuko Wa Abbot
CCM yajibu mashambulizi ya operesheni UKUTA ya Chadema