Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg amezua kizazaa nchini humo baada ya kunaswa na kamera akicheza ‘game’ ndani ya Bunge wakati wabunge wakichangia mjadala muhimu.

Erna Solberg alinaswa akiwa ameiweka akili yake kwenye mchezo maarufu unaojulikana kama ‘Pokemon Go’ Jumanne iliyopita wakati kiongozi wa chama kikongwe zaidi nchini humo cha ‘Liberty Party’, Trine Skei Grande akichangia mjadala.

Kwa mujibu wa mtandao wa Independent, hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa shughuli za serikali bungeni kuzidiwa na uhondo wa game hilo kwenye simu yake ya kupapasa wakati wa kazi kwani mwezi Agosti alifikia hatua ya kusimamisha vikao vya kiofisi ili aweze kumaliza kiu yake kwa mchezo huo akiwa katika mji wa Slovakia.

Picha za mchezo wa Pokemon Go

Picha za mchezo wa Pokemon Go

Hata hivyo, baada ya kusambaa picha zinazomuonesha Solberg anacheza game bungeni, Grande aliyekuwa akitoa mjadala wake bungeni muda huo, aliamua kumtetea kupitia mtandao wa Twitter akieleza kuwa haoni tatizo kwani wanawake wanaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

“Alinisikia nilichokuwa nazungumzia [bungeni] kwa sababu kama ujuavyo sisi wanawake tunaweza kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja,” ilisomeka tweet yake.

Picha: Luis Suarez Achukua Jukumu La Kulinda Lango
Video: Mjema aipa Halmashauri miezi 3 kurekebisha soko la Kigogo Fresh, apiga marufuku ushuru