Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ameongoza  waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Mzee Xavery alifariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

 Waziri Mkuu ametoa pole kwa wanafamilia na kuwaomba waendelee kumuombea marehemu apumzike mahala pema peponi.

Amesema kuwa msiba huo ni mzito, hivyo anawaomba wanafamilia wawe watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Aidha, Majaliwa amemuhakikishia Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kwamba Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.

“Serikali imetoa ndege kwa ajili ya kusafirisha msiba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ataiwakilisha Serikali katika mazishi hayo,” alisema.

Kwa upande wake, Mizengo Pinda aliwashukuru viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi kwa kutenga muda wao na kwenda kumfariji kufuatia msiba huo mzito. “Kuondokewa na baba mzazi au mwanafamilia yeyote si jambo dogo.”alisema Pinda.

Mzee Xavery anatarajiwa kuzikwa kesho (Alhamisi, Desemba Mosi, 2016) katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Mlele mkoani Katavi. Marehemu ameacha mke, watoto wanane, wajukuu 54 na vitukuu

TPDC: Kampuni ya Dangote wamepotosha umma
Simbachawene apigilia msumali maadhimisho ya walemavu