Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika siku 100 umeweka historia kubwa ya mafanikio ya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na Dar24 Media yaliyofanyika Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mulamula amesema wizara yake imepewa bajeti ya kimkakati ya kuongeza uchumi. Amesema wanajenga vituo vya vitega uchumi katika mataifa mbalimbali duniani ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Amesema amaeneo ambayo watatumia fedha hizo kujenga majengo ya vitega uchumi ni pamoja na Nairobi nchini Kenya, Kigali nchini Rwanda, Uarabuni na Saudia.

“Bajeti tumepewa na pesa imeshaanza kutolea, haijawahi kutokea. Kwakweli mimi kama Waziri nimefarijika sana, katika siku hizo 100 nimeona mafanikio makubwa sana, na niseme nikirudi tena mwaka mmoja mtaona mambo yatakavyokuwa mazuri zaidi,” alisema Waziri Mulamula.

Aidha, alizungumzia hatua kubwa iliyofikiwa katika kuimarisha ujirani mwema na nchi za Afrika Mashariki, akieleza jinsi ambavyo vikwazo vya kibiashara vilivyoondolewa katika mipaka ya Tanzania na Kenya pamoja na nchi nyingine.

Katika hatua nyingine Balozi Mulamula alizungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania kuhusu chanjo ya corona, ushiriki wa vyombo vya habari na wadau wa maendeleo.

Angalia mahojiano zaidi hapa chini:

TMA: Upepo mkali kuathiri maeneo yafuatayo
Acha kufanya mambo haya uwe mjasiliamari mkubwa