Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wafanyabiashara waliokimbilia Nakonde nchini Zambia, kwa maelezo ya kuwa huko kuna unafuu wa kodi kuliko Tunduma nchini Tanzania warejee na malalamiko yao yatafanyiwa kazi.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi Mjini Tunduma wakiwemo wafanyabiashara katika mpaka huo wa Tanzania na Zambia walioeleza kero zao mbalimbali.

Wewe Mtanzania wala usiikimbie nchi yako tutarekebisha yale yaliyomatatizo lakini kama umepata fursa ya kuwekeza wekeza inaruhusiwa, lakini usiikimbie nchi yako sababu ya matatizo hayo tutayarekebisha,” amesema Dkt. Nchemba.

Tanzania inaheshima ya kuokoa nchi zote hizi za majirani hatuwezi tukasindwa kutenda haki kwa mambo ya wananchi wetu hayo yote tumeyachukua tutayafanyia kazi naomba mridhie tumeyapokea” amesema Dkt. Nchemba

Mukoko Tonombe aomba radhi Young Africans
Benki mpya ya TCB yashiriki maonesho ya biashara na teknolojia ya madini Shinyanga