Zaidi ya watu 500 wamefariki baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Richter 7.9, lililoyakumba maeneo kadhaa ya katikati mwa nchi ya Uturuki na kaskazini magharibi mwa nchi Syria.

Vifo hivyo, vilitokea bada ya majengo kuporomoka huku vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwatafuta waathirika waliokwama kwenye vifusi.

Moja kati ya uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi. Picha ya Eos.org

Taarifa zaidi zinasema, watu wengine zaidi ya 600 wamejeruhiwa na msaada wa kimataifa unahitajika katika kukabiliana na matokeo mabaya ya tetemeko hilo, ambalo limefika hadi nchi za Cyprus na Lebanon.

Uturuki, ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikikumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, ambapo mwaka 1999 watu 17,000 walifariki kutokana na tukio kama hilo lilipopiga mji wa Izmit na lile la 2011 katika mji wa Van lililouwa watu 500.

Kichuya: Endeleeni kunizomea
Bungeni: Kampuni za simu zatakiwa kufidia wateja