Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa mgonbea urais wa Chadema, Edward Lowassa aliwavuruga na kufifisha matarajio yao.

Zitto amesema kuwa awali chama chake kilikuwa kimefanya mazungumzo na wabunge takribani 50 waliokuwa wamekubali kujiunga na chama hicho wakitokea CCM na Chadema, lakini baada ya Lowassa kuingia Chadema mpango huo ulivurugika.

Alisema kuwa Lowassa alikuwa na nguvu kubwa na kwamba haikutabirika kama angeingia Chadema hivyo uwepo wake ndani ya chama hicho uliwafanya wabunge wote 50 waliokuwa wamepanga kuhamia ACT – Wazalendo kushindwa kuendelea na mpango wao kama alivyokuwa ameahidi kabla ya uchaguzi.

“Wabunge wengi walikubali kuungana nasi, wamo wa CCM na wabunge wa upinzani. Lakini upepo wa Lowassa uliwabadilisha na hili tusingeweza kulithibiti kwa kipindi kile,” alisema.

Kupitia taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye ‘Mwananchi’ , Zitto aliongeza kuwa nguvu hiyo ya Lowassa iliyokuwa ikiungwa mkono na Ukawa ilisababisha ACT-Wazalendo kushindwa kupata viti vingi vya ubunge kama walivyotarajiwa.

Picha: Wafungwa Wanawake washiriki shindano la Urimbwende ‘Miss Criminal’
CCM Wazungumzia Taarifa Kuwa Wamekubali Maalim Seif Aapishwe Kuwa Rais Wa Zanzibar