Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma amesema kuwa mustakabali wa chama tawala nchini humo cha African National Congress (ANC) upo katika hatari kubwa ya mpasuko.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wajumbe wa chama hicho waliokutana kumchagua mrithi wake atakayekiongoza chama hicho.

Zuma amesema kuwa kwasasa kuna haja ya kuunganisha nguvu pamoja na kumchagua kiongozi atakayehakikisha anasimamia vyema misingi ya chama hicho ili kuweza kukinusuru na mpasuko ambao umekuwa ukinjionyesha zahiri.

Aidha, mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mzozo uliojitokeza kuhusu nani anatakiwa kupiga kura na nani harusiwi kupiga kura za kumchagua mrithi wa kiongozi huyo.

Ushindani mkubwa uko kwa wagombea wakuu wawili wanaopigiwa upatu kumrithi kama kiongozi wa chama hicho ni makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa, na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa Zuma.

Hata hivyo, Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa, huku kikiandamwa na migogoro ya ndani.

DC Kasesela awataka Chadema kujitathmini
Waliohama vyama mikononi mwa Takukuru